9 Februari 2016 - 20:39
Umoja wa Mataifa waituhumu serikali ya Syria kwa mauaji

Ushindi wa jeshi la Syria dhidi ya magaidi, umepelekea Marekani na washirika wake ambao wamekuwa wanaunga mkono magaidi hao, kufanya kikao cha kujadili jinsi ya kuwasaidia magaidi hao ikibidi watume majeshi yao kuwasaidia, huku wakijaribu kuonyesha kwenye vyombo vya habari kwamba wao wanatetea wananchi.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa juu ya Syria imetoa mapendekezo ya kutaka vitangazwe vikwazo dhidi ya maafisa wa ngazi ya juu wa Syria wanaowajibika na kile kinachodaiwa kuwa ni uhalifu wa mauaji ya wafungwa.

Ripoti ya tume maalum ya uchunguzi juu ya Syria pia imetaja juu ya mauaji ya watu wengi yaliyofanywa na kundi la kigaidi la Daesh pamoja na kundi linalofungamana na mtandao wa Alqeda nchini Syria la Al Nusra Front lakini ripoti hii imeacha makundi mengine ya kigaidi yanayofanya jinai zake nchini Syria.

Kimsingi jopo hilo la Umoja wa Mataifa limeweka bayana kwenye ripoti yake kwamba makundi mbali mbali yamehusika kuua maelfu ya wafungwa tangu vita vya vilipoanza nchini Syria mwaka 2011 mnamo mwezi Marchi. Ripoti hiyo imetolewa sambamba hapo jana na ziara ya kansela wa Ujerumani Angela Merkel mjini Ankara ambako walifanya mazungumzo na waziri mkuu Ahmet Davutoglu na baadae kukutana na waandishi wa habari na kutangaza kilichoafikiwa katika mkutano wao.

Miongoni mwa masuala makubwa yaliyotajwa kufikiwa ni pamoja na ushirikiano wa nchi hizo mbili Uturuki na Ujerumani kutafuta njia za kuishinikiza jumuiya ya kujihami ya Nato kuwa mwangalizi katika mpaka kati ya Uturuki na Ugiriki kwenye eneo la bahari ya Mediterrenia. Kansela Merkel pia alibaini kwamba matumizi ya nguvu yanayoonyeshwa na Urusi na Syria dhidi ya magaidi katika mkoa wa Aleppo yanabidi kukomeshwa. Wakati huohuo imearifiwa kwamba jeshi la Syria limekiteka kwa mara nyingine kijiji cha pili katika mkoa wa Aleppo na kulifanya jeshi hilo na washirika wake katika mapambano kukaribia kabisa kufikia mpaka wa Uturuki na kuwarudisha nyuma magaidi wanaoungwa mkono na Ulaya na Marekani pamoja na washirika wake wa kiarabu.

Ushindi wa jeshi la Syria dhidi ya magaidi, umepelekea Marekani na washirika wake ambao wamekuwa wanaunga mkono magaidi hao, kufanya kikao cha kujadili jinsi ya kuwasaidia magaidi hao ikibidi watume majeshi yao kuwasaidia, huku wakijaribu kuonyesha kwenye vyombo vya habari kwamba wao wanatetea wananchi.

Wakati huohuo maelfu ya wasyria wanaoyakimbia mapigano wamekusanyika katika mpaka wa Uturuki huku serikali ya Uturuki ikikhofia kwamba mapigano makali yanayoongezeka katika mkoa wa Aleppo yanaweza kuchochea watu wengi kuzidi kuyakimbia makazi yao na kukimbilia kwenye mpaka huo wa Uturuki.

Serikali ya Uturuki inakhofia kwamba mapigano makali yanayoendelea Aleppo yanaweza kuifanya idadi ya wanaokimbilia kwenye mpaka wake ikafikia watu 60,000 ameeleza hayo naibu waziri mkuu Nurman Kurtulmus akitaja kuwa hilo litakuwa ni tukio kubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa. Kundi kubwa kabisa la wakimbizi wengi wakiwa ni wanawake na watoto wamelazimika kupiga kambi katika mpaka wa Onvupinar ambao bado umefungwa lakini wakifunguliwa watu walio na mahitaji ya dharura ya huduma za afya.

Mapigano makali kaskazini mwa mkoa wa Aleppo yaliyochochewa na mashambulizi ya wiki nzima ya vikosi vya serikali vikisaidiana na ndege za kivita za urusi dhidi ya magaidi nchini Syria yameshababisha kukomboa miji mingi iliyokuwa chini ya himaya ya maigaidi na hatimaye wananchi wa miji hiyo kuanza kuhisi matunda ya amani.

Mwisho wa habari/ 291